Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la soka nchini(Tff) Oscar Milambo ameteuliwa na shirikisho la soka Duniani(Fifa) kwenye kamati maalumu kwa ajili ya kutengeneza mitaala na moduli za mafunzo ya kozi zote za CAF kuanzia Diploma D mpaka A.
Milambo amekua mmoja wa maafisa 6 barani Afrika kuteuliwa kushika wadhifa huo adhimu ambapo atapata fursa ya kuliwakilisha Taifa.
Kocha huyo ni mmoja ya makocha wachache wasomi nchini ambapo pia alipata nafasi ya kuifundisha timu ya vijana chini ya miaka 17 katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika yaliyofanyika nchini mwaka jana.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.