Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa shirikisho la kabumbu barani Afrika “CAF” limemfuta kazi aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Chelsea Didier Droga kutokana na kushindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo nguli Afrika Mamadou Gaye, CAF wametengua uteuzi wa Didier Drogba kama mshauri wa Rais wa CAF Ahmad Ahmad.
Ikumbukwe kuwa July 2019 staa huyo (Drogba) na staa wa zamani wa Barcelona na Cameroon Samwel Eto’o waliteuliwa kuwa washauri wa Ahmad Ahmad lakini Drogba hajatoa mchango wowote katika kazi hiyo na wala hajawahi hudhuri shughuli yoyote ya CAF ikiwemo mechi hata moja ya AFCON 2019 toka alipoteuliwa katika ngazi hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.