Site icon Sports Leo

Cas Yaibuka Kesi ya Morrison

Mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa kesi za michezo (Cas) wamesema kwamba kesi ya klabu ya Yanga sc dhidi ya mchezaji Benard Morrison itasikilizwa kuanzia tarehe 3 mwezi juni baada ya kujiridhisha kuwa kuna kesi ya kusuluhisha.

Cas wamewataka Yanga sc na Morrison kuwasilisha nyaraka za ushahidi ama kesi isikilizwe kwa kutumia nyaraka za awali ili kutoa hukumu ya kesi hiyo.

Kesi hiyo imechelewa kusikilizwa kiasi cha mashabiki wengi kudai ni ujanja wa viongozi wa Yanga sc kuficha udhaifu wao huku Yanga sc wakisema kesi imecheleweshwa baada ya mlalamikiwa Benard Morrison kudai kuwa kesi hiyo ilidishwe nchini ili isikilizwe na mamlaka za ndani ambapo shauri hilo limekataliwa na Cas.

Exit mobile version