Taarifa za kusikitisha ni kwamba mchezaji wa klabu ya Simba sc Cletous Chama amefiwa na mke wake anayefahamika kwa jina la Mercy baada ya kuugua kwa muda mfupi nchini Zambia.
Noel Mwandila aliyekua kocha wa klabu ya Yanga sc amethibitisha taarifa hizo huku akisema msiba upo mjini Lusaka japo hafahamu kiundani zaidi lakini ni taarifa zilizosambaa nchinin humo.
Chama ataukosa mchezo wa ligi kuu nchini dhidi ya Namungo Fc ili kuhudhuria msiba huo mkubwa huku klabu ya Simba sc ikitarajiwa kukaa na benchi la ufundi baada ya mechi ya leo kujua cha kufanya.