Kinda wa Kiholanzi Tahit Chong amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kukipiga katika klabu ya Manchester United huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi mpaka mwaka 2022.
Kinda huyo mkataba wake wa awali ulikua unaisha mwezi june mwaka huu na kuzivutia timu kadhaa kama Inter Milan huku makubaliano na United yalikua yakilegalega kabla ya kusaini dili hilo.
Chong alijiunga na United mwaka 2016 na alicheza mechi ya kwanza ya kikosi cha wakubwa mwezi january mwaka 2019 dhidi ya Reading katika kombe la Fa alisema ni ndoto kwake kujiunga na timu hiyo na anafuraha kuongeza mkataba klabuni hapo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.