Site icon Sports Leo

EMENALO kwenye mipango ya Newcastle United

Uongozi wa klabu ya Newcastle United unamtazama mkurugezi wa zamani wa ufundi wa Chelsea Michael Emenalo kuwa mkurugenzi wao mpya wa michezo kwenye timu yenye makzi yake St James’ Park Uingereza.

Emenalo alijiunga na Chelsea mwaka 2007  kama sehemu ya benchi la ufundi lililokuwa chini ya Avram Grant akiwa skauti mkuu kabla ya kupandishwa kuwa kocha msaidizi mwaka 2010 alipoondoka Ray Wilkins.Mnamo mwaka 2011 aliteuliwa rasmi na klabu hiyo kuwa mkurugenzi wa ufundi.

Mnigeria huyo alijiuzuru mwaka 2017 katika nafasi yake kutokana na muingiliano wa kimadalaka kati yake na mtendaji Maria.

Alipokuwa Chelsea alileta mabadiliko makubwa katika akademi ya klabu hiyo,kuboresha idara ya usajili pamoja na kuisuka vizuri timu ya wanawake wa Chelsea.Anakumbukwa kwa kuwezesha sajili kubwa kama Eden Hazard,Kevin De Bruyne,Juan Mata,Cesc Fabregas,Diego Costa na Thibaut Courtious kutokana na uwezo wake mkubwa wa kung’amua vipaji mbalimbali.

CV yake imewafanya mabosi wa Newcastle kumuona mtu sahihi wa kuipeleka timu yao kule wanakotaka kutokana na mafanikio makubwa aliyopata Chelsea ikiwamo mataji kama ya ligi kuu mara tatu,Ubingwa wa Ulaya mara mbili,kombe la FA mara nne na kombe moja la ligi.

Bado inasubiriwa kuona kama kweli mabosi wa Newcastle watamuajiri Emenalo kutokana na kuhusishwa na watu wengine kama mkurugenzi wa zamani wa michezo wa RB Leipzig Mjerumani Ralf Rangnick.

Exit mobile version