Site icon Sports Leo

Fei Toto Aimaliza Ruvu Shooting

Mabao mawili ya Feisal Salum dakika za 23 na 32 na lile la Saido Ntibanzokiza yalitosha kuipa Yanga sc alama tatu dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu nchini.

Matokeo ya mwisho ya mabao 3-2 yalionekana kutowafurahisha wanajangwani hao kiasi cha kusababisha mashabiki kumlaumu Metacha Mnata kutokana na kuruhusu bao la kizembe la pili lililowatia hofu mashabiki hao.

Mabadiliko ya kumtoa Mukoko Tonombe yalisababisha Yanga sc kukosa nguvu eneo la katikati huku kuingia kwa Emmanuel Martin kulisababisha Ruvu kuwa na madhara eneo la ushambuliaji.

Exit mobile version