Klabu ya Yanga SC kwa sasa rasmi imeungana na klabu ya Simba kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya klabu Bingwa Afrika (CAF Champion League) msimu wa 2021/22 baada ya kuifunga Ihefu kwa magoli 2-0 na kufikisha pointi 73 na kuwa na uhakika wa kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom.
Wakati Simba na Yanga wakiiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya CAF Champion League vilabu vya Azam FC na Biashara United zenyewe zitaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kombe la shirikisho (CAF Confederation Cup) baada ya kuwa na uhakika wa kumaliza nafasi ya 3 na 4 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom.