Site icon Sports Leo

Feisal,Mukoko Kuwakosa Prisons Fc

Afisa habari wa klabu ya Yanga sc Hassan Bumbuli amesema kuwa klabu hiyo itawakosa viungo wake mahiri Feisal Salum na Mukoko Tonombe kutokana na kadi tatu za njano walizozipata katika michezo ya ligikuu nchini.

“Tunaenda kuwavaa Prisons tukiwakosa nyota wetu watatu ambao watakuwa wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano, benchi la ufundi linajua na tunaamini Kocha amekuwa na mpango wake kwa Wachezaji waliopo,”
Amesema adhabu hiyo ni ya kikanuni na licha ya kukosena kwa nyota hao kikosi bado kiko imara kwenye maeneo yote kwani kuamna viungo na washambuliaji wengine kikosini.
“Eneo la kiungo japo Mukoko na Feisal wamekuwa chaguo la kwamza kikosini kwa muda mrefu, lakini tuna machaguo mengine kama Zawadi Mauya, Carlinhos na Haruna Niyinzima, na kwenye ushambuliaji pia kuna machaguo mengine hivyo kikosi bado kiko imara sana,”.

 

Pia Bumbuli amesema kuwa pamoja na viungo hao pia mshambuliaji Michael Sarpong nae atakosekana katika mchezo huo kutokana na kadi tatu kama wenzake.

Exit mobile version