Site icon Sports Leo

Gerd Muller aaga dunia

Gwiji la soka nchini Ujerumani Gerd Muller na klabu ya soka ya Bayern Munich amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 75 taarifa kutoka klabu yake hiyo ya zamani ikithibitisha.

Mshindi huyo wa kombe la dunia mwaka 1974 akiwa na kikosi cha Ujerumani anatajwa kuwa mmoja kati ya washambuliaji hatari kuwahi kutokea.

Muller anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika michuano mimoja ya kombe la dunia akifunga magoli  10 mwaka 1970 akichukua pia tuzo ya Ballon d’Or mwaka huo.

Exit mobile version