Site icon Sports Leo

Giroud atua Ac Milan

Klabu ya Ac Milan imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Olivier Giroud akitokea Chelsea alikohudumu kwa miaka mitatu.

Giroud alijiunga na Chelsea mwaka 2018 akitokea Arsenal kwa dau la paundi milioni 18.

Mshambuliaji huyo ametwaa mataji matatu akiwa na Chelsea ambayo ni FA cup, Europa league na UEFA champions ligi ametua Milan kwa ada ya paundi milioni 1.6 tu.

Giroud aliandika katika mtandao wake wa twitter ”ushindi wetu kwenye FA, Europa league na UEFA champions league ulikuwa wa kipekee sana, kwenye nyote the blues,wachezaji wenzangu na makocha wote asanteni sana kwa nyakati hizi nzuri”.

Exit mobile version