Kesho utakua ni mtihani wa kwanza wa kocha Didier Gomez katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa kiporo utakaofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Humo.
Gomes aliyesajiliwa na Simba sc akitokea El-Merreikh ya Sudan atakua na kibarua kigumu cha kuchukua alama tatu muhimu dhidi ya timu hiyo iliyopanda daraja la ligi kuu msimu huu.
“Utakuwa mchezo mgumu lakini tupo tayari kupambana ni muhimu sana,tuna michezo mitatu mkononi na tunatakiwa kushinda michezo yote ili kupunguza alama na timu iliyopo kileleni na mchezo wa kwanza ni kesho.”Alisema Gomez
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.