Site icon Sports Leo

Grealish atakiwa Man City

Mchezaji wa Kiingereza Jack Grealish anahusishwa kujiunga na klabu ya Man city baada ya mabingwa hao wa Uingereza kuwasiliana na klabu ya sasa ya kiungo huyo Aston villa na kuanza mazungumzo ya kusajili mchezaji huyo katika viunga vya Eithad.

Nahodha huyo wa Aston villa anathaminishwa na klabu yake kwa dau la paundi 100m na Aston villa imewaambia City kulipa kiasi hicho ilikumruhusu kiungo huyo fundi kujiunga na klabu ya Man city yenye maskani yake jijini Manchester.

Man city itasubiria hadi kumalizika kwa michuano ya Euro 2020 ili kumsajili mchezaji huyo anayehusudiwa sana na kocha wao Pep Gudiola.

Exit mobile version