Site icon Sports Leo

Gsm Wachangia Matibabu Ya Mdamu

Bosi wa makampuni ya Gsm Gharibu Said Mohamed amejitolea kiasi cha Shilingi milioni 6 kuchangia matibabu ya mchezaji wa timu ya Polisi Tanzania Gerrad Mathias Mdamu aliyevunjika miguu yote miwili baada ya kupata ajali ya basi wakati wakitokea mazoezini na klabu hiyo.

Awali mchezaji huyo alipata matibabu katika Hospitali ya Kcmc mjini Moshi lakini baada ya hali kutotengemaa alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako bado anaendelea na matibabu huku michango ya wadau ikihitajik kufanikisha matibabu ya mchezaji huyo kutokana na gharama kuwa kubwa.

Mchango wa bosi huyo anayeifadhili klabu ya Yanga sc umesemwa na Haji Manara wakati akihojiwa na redio ya Wasafi Fm huku naye akichangia kiasi cha shilingi laki saba kama mchango wake binafsi.

Exit mobile version