Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwaka 2020/21 wa ligi kuu ya Uingereza kwa kupata kura nyingi kutoka kwa makocha wenzake baada ya kutwaa tuzo hiyo ( The League Managers’ Association manager of the year. – LMA )
Makocha wengine watano ambao walikuwa kwenye kinyang’anyiro hiko ni pamoja na Marcelo Bielsa (Leeds), Daniel Farke (Norwich), Emma Hayes (Chelsea Women), David Moyes (West Ham) na Brendan Rodgers (Leicester).
Kocha huyo ametwaa tuzo hiyo baada ya kuiwezesha klabu ya Manchester City kutwaa taji la tatu la ligi kuu nchini Uingereza ndani ya miaka yake mitano ya kuifundisha klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.