Site icon Sports Leo

Inter yaichomolea Chelsea kwa Lukaku

Klabu ya soka ya Inter Milan ya Italia imeipiga chini ofa ya klabu ya Chelsea kwaajili ya kumnunua mshambuliaji wake raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku.

Chelsea imepeleka ofa ya kitita cha Euro milioni 100 pamoja na kumjumuisha beki wake Marcos Alonso lakini ofa hiyo imekataliwa mara mojan na mabingwa hao wa Seria A, na kusema kuwa Lukaku hauzwi kwani ni mchezaji wao muhimu na yupo kwenye mipango yao.

Inter inagoma kuuza mchezaji mwingine muhimu kwenye kikosi chao baada ya kumuachia beki Hakimi kujiunga na PSG,hivyo kama kweli Chelsea inamtaka Lukaku itawalazimu kuongeza ofa yao kuwajaribu mabingwa wao kumuacha mshambuliaji huyo .

Chelsea imehamia kwa Lukaku baada ya mazungumzo yao na Dortmund kwa Halaand kuwa magumu huku dili hilo likihitaji pesa nyingi zaidi.

Exit mobile version