Wenyeji wa michuano ya mataifa ya Afrika (Afcon 2024) timu ya Taifa ya Ivory Coast imeanza vyema michuano hiyo baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Gambia katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo uliofanyika nchini humo na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki.
Mabao ya Ivory Coast yalifungwa na Christian Kouamé (45′) pamoja na Seko Fofana (85′) na kupeleka kilio kwa Gambia inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga sc Tom Saintfiet ambaye ni raia wa Ubelgiji.
Ivory Coast pamoja na ushindi huo bado haikua na kiwango kilicho bora katika mchezo huo kinyume na matarajio ya mashabiki wengi waliokua na imani kuwa wenyeji hao wataonyesha soka safi kutokana na maandalizi makubwa waliyofanya.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Msimamo wa kundi A sasa wenyeji wanaongoza wakiwa na alama tatu huku Nigeria na Equatorial Guinnea kila mmoja akiwa na alama moja moja na Gambia akiwa mwishoni mwa msimamo akiwa hana alama.