Site icon Sports Leo

Japan yajitoa uandaaji klabu bingwa dunia

Nchi ya Japan imejitoa kuandaa michuano ya klabu bingwa ya dunia iliyopangwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu kutokana na vikwazo vya ugonjwa wa UVIKO-19 ndani ya nchi hiyo.

Shirikisho la soka duniani FIFA limesema kuwa wamepokea taarifa kutoka chama cha soka cjha Japan(JFA) leo alhamisi kuwa hawatoweza tena kuwa wenyeji wa michuano hiyo.Michuano hiyo hushirikisha mabingwa wa mabara mbalimbali ngazi ya vilabu.

FIFA wamesema kuwa watatoa taarifa mapema ya mbadala wa Japan katika kuandaa mashindano hayo.

Japan walioandaa mashindano ya Olimpiki na ile ya Olimpiki ya walemavu majira haya ya kiangazi,wamejikuta katika hali ya dharura kitaifa kutokana na kukabiliwa na wimbi kubwa la UVIKO-19.

Bayern Munich ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo walipoishinda Al Ahly ya Misri mwaka 2020 na mwaka huu ni mwaka wa tisa wa mashindano hayo huku Afrika wakiwakilishwa tena na Al Ahly na Chelsea wakiiwakilisha bara la Ulaya.

 

Exit mobile version