Site icon Sports Leo

Kagere awapa Simba SC pointi 3 Dodoma

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara hatimaye wamepata ushindi wao wa kwanza msimu huu baada ya kuitandika Dodoma Jiji kwa bao 1-0 katika mchezo wa vuta nikuvute kwenye dimba la Jamhuri Dodoma.

Mshambuliaji wa Kinyarwanda Meddie Kagere ndiye aliyekua shujaa wa mchezo huo na kwa timu yake baada ya kupachika bao pekee dakika ya 70 akimalizia pasi nzuri ya kichwa kutoka kwa Chris Mugalu na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa klabu hiyo waliofurika kushuhudia mchezo huo.

Dodoma Jiji walionekana kutumia nguvu sana kuwakabili Simba kiasi cha kupelekea Simba kuwapoteza wachezaji wake Kenedy Juma,Tadeo Lwanga na Pape Sakho kutokana na majeruhi,mshambuliaji wa Dodoma Jiji Anwar Jabir dakika ya 41 alioneshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko beki wa kati wa Simba Kenedy Juma na kuipunguzia makali timu yake.

Simba kwasasa wamefikisha alama 4 katika michezo miwili ya ligi kuu msimu huu na ushindi wa leo utawapa morali kuelekea mashindano ya klabu bingwa Afrika hatua ya pili ya mtoano kufuzu makundi dhidi ya Jwaneng FC ya Botswana kati Oktoba 15-17.

Katika mchezo mwingine wa ligi kuu uliofanyika hii leo Ruvu Shooting imepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Biashara United ugenini.

Exit mobile version