Site icon Sports Leo

Kane agomea mazoezi Spurs

Mshambuliaji na nahodha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Kane ameshindwa kuonekana kwenye mazoezi ya timu hiyo hivi leo mara baada ya kumalizika kwa likoizo yake.

Mchezaji alipewa likizo ndefu kufuatia kushiriki kwake kwenye michuano ya Euro 2020 akiwa na timu ya taifa ya England ambapo walifika hatua ya fainali,na alitarajiwa kuanza kujiunga na wenzake hii leo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Hatua hiyo inatajwa ni kushinikiza uhamisho wake kwenda klabu ya Manchester city ambayo wanamhitaji kuziba pengo la Aguero aliyetimkia Barcelona.Kane alifikia makubaliano na Spurs kuruhusiwa kuondoka katika dirisha hili lakini timu hiyo inaonekana kuweka ngumu kumruhusu kuondoka baada ya kukataa dau la paundi milioni 100 kutoka Man city.

Hivyo kitendo cha kutokuonekana ni ishara ya kushinikiza kuondoka baada ya Spurs kukiuka makubalioano yao.

 

Exit mobile version