Home Soka Karia Apokea Jezi za Yanga Sc na Simba Sc

Karia Apokea Jezi za Yanga Sc na Simba Sc

by Sports Leo
0 comments

Rais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania Wallace Karia amepokea jezi kutoka klabu za Simba Sc na Yanga sc kuelekea katika mechi za timu hizo za robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika itakayofanyika wiki ijayo siku za ijumaa na Jumamosi.

Karia akiwa na Athuman Nyamlani ambaye Makamu wake wa Kwanza walipkea jezi hizo kutoka kwa Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewakabidhi jezi hizo kwa ajili ya mechi ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundown itakayofanyika siku ya Jumamosi Machi 30 katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

banner

Pia karia alishapokea Jezi ya klabu ya Simba sc ambayo nayo itakua na mchezo wa robo fainali dhidi ya Al Ahly utkaofanyika pia katika uwanja huo siku ya Ijumaa machi 29 saa tatu kamili usiku.

Hii ni mara ya kwanza kwa klabu za Tanzania kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa ikiwa timu mbili kwa mpigo zimevuka hatua hiyo ikiwemo Yanga sc ambayo imevunja rekodi baada ya kufuzu kwa mara kwanza hatua hiyo baada ya miaka 25 kupita.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited