Site icon Sports Leo

Kibabage Bado Kidogo Simba sc

Beki wa Difaa El Jadidi Mtanzania Nickson Kibabage tayari yupo nchini Tanzania na inaelezwa kuwa Klabu ya Simba ina mpango wa kumsajili beki huyo anayecheza mbavu ya kushoto kuwa msaidizi wa Mohamed Hussein’
Iwapo Simba sc watamkosa beki huyo ambaye hivi sasa anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Youssofia Berrechid ya Morocco mwisho wa msimu huu basi itaangalia uwezekano wa kumsajili beki wa kushoto wa KMC, Brayson David.

 

Tayari klabu hiyo ipo mbioni kuachana na Gadiel Michael baada ya kushindwa kuonyesha kiwango kumpa changamoto Mohamed Hussein.

Exit mobile version