Site icon Sports Leo

Kipa Aigle Noir atua Yanga

Golikipa Mtanzania aliyekua anakipiga katika klabu ya soka ya Aigle Noir ya Burundi Eric Johora amejiunga na klabuj ya soka ya Ynga kwa mkataba wa miaka miwili.

Johora aametua Jangwani kuchukua mikoba ya Metacha Mnata aliyeachwa baada ya kumalizika kwa mkataba wake.

Mchezaji huyo alionekana kwa mara ya kwanza alipokuja nchini na timu ya Aigle Noir kucheza mechi ya kirafiki na Yanga wiki ya Mwanachi na kuonesha kiwango safi kilichowavutia mabosi hao wa Jangwani na kuanza kumfuatilia hadi kufikia hatua ya kumsajili.

Exit mobile version