Site icon Sports Leo

Kipa la MALI latua JANGWANI

Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kuipata saini ya mlinda mlango wa kimataifa wa Mali Djigui Diarra 26, kukipiga kwa mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania.

Golikipa huyo amesajiliwa kutoka klabu ya Stade Malien ya kwao Mali aliyokua akiichezea tangu mwaka 2006.

Diarra anakuja kuchukua nafasi ya magolikipa Metacha Mnata na Farouk Shikalo katika kikosi cha kwanza wanaohusishwa kuondoka kwa wanachi hao.

Exit mobile version