Home Soka Kisa Al Ahly,Simba Sc Yajichimbia Zanzibar

Kisa Al Ahly,Simba Sc Yajichimbia Zanzibar

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba Sc imeamua kuweka kambi maalumu ya maandalizi visiwani Zanzibar Kuiwinda Al Ahly katika mchezo ujao wa ligi ya mabingwa barani Afrika  utakaopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam siku ya Ijumaa Machi 29.

Kikosi hicho cha Simba sc tayari kimeondoka jijini Dar es salaam mapema hii leo kikiwa na mastaa wake wengi wa kikosi cha kwanza isipkua Cletous Chama ambaye ameitwa katika timu ya Taifa ya Zambia na Mohamed Hussein,Aishi Manula,Kibu Dennis na Kennedy Juma ambao wameitwa katika timu ya Taifa ya Tanzania ambayo imesafiri nchini Azerbaijan kwa ajili ya michezo ya kirafiki ya Fifa.

Kambi hiyo ni mapendekezo ya kocha Abdelhack Benchika ambaye ametaka timu hiyo ijichimbie visiwani humo kwa ajili ya kambi hiyo ya siku takribani kumi kuwawinda Al Ahly katika mchezo huo wa hatua ya robo fainali ambao mpaka sasa umevuta hisia za mashabiki nchini.

banner

Katika msafara huo mastaa kama Ayoub Lakred,Shomari Kapombe,Hussein Kazi,Babacar Sarr,Fabrice Ngoma na Pa Omar Jobe walikua ni sehemu ya msafara huo ambao umeondoka Dar es salaam kwa boti kuelekea visiwani humo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited