Klabu ya Chippa United ya ligi kuu nchini Afrika Kusini, imethibitisha kuteuliwa kwa Mbelgiji, Luc Eymael (61) kama kocha wao Mkuu mpya inayoshiriki ligi kuu nchini humo.
Mkongwe huyo katika bara hili ambaye amesimamia vilabu kama AS Vita, AFC Leopards, Rayon Sports, Al Merriekh, Free State Stars, Polokwane City, Yanga SC na zingine; Amesaini Mkataba wa Hadi mwisho wa Msimu huu wa DStv Premiership ambao upo mzunguko wa nane.
Baada ya Mechi hizo nane, Chippa inashika Nafasi ya 14 kwa pointi tano huku ikiwa imepata ushindi Mara moja, Sare Mbili na Vipigo Vitano.