Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania Habib Kyombo amekamilisha rasmi uhamisho wa kujiunga wa timu ya Mamelod Sundowns inayoshiriki ligi kuu ya Afrika kusini kwa mkataba wa miaka minne.
Kyombo 19 alifahamika katika ramani ya soka alipokua anaichezea timu ya Mbao Fc ya mwanza na baadae akajiunga na Singida United na kupata nafasi ya kufanya majaribio katika timu hiyo ambapo alifuzu lakini alishindwa kukamilisha usajili mpaka dirisha la usajili lilipofunguliwa rasmi.
Katika barua aliyoiandika mchezaji huyo katika mtandao wake wa kijamii alithibitisha kukamilisha usajili na kuwashukuru watu mbalimbali ikiwemo timu yake ya zamani ya Singida united na kampuni iliyomsaidia kukamilisha usajili ya Shadaka sports managements.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.