Inadaiwa klabu ya Simba sc ipo mbioni kuachana na mchezaji Junior Lokosa kutokana na kuonyesha kiwango duni katika kikosi hicho.
Lokosa licha ya kusajiliwa kwa matumaini kibao ameshindwa kulishawishi benchi la ufundi la klabu hiyo kutokana na kucheza chini ya kiwango huku akiwa na uoga wa kuumia tena baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha.
Mchezaji huyo amecheza mechi moja pekee katika michuano ya Simba sc Super Cup huku ikidaiwa anaenda ama nchini Norway au nchini Afrika ya kusini ambapo amepata ofa.