Site icon Sports Leo

Lukaku: Inter pokeeni ofa ya Chelsea

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji na klabu ya soka ya Inter Milan ya Italia Romelu Lukaku ameiambia klabu yake hiyo kupokea ofa itakayoletwa na Chelsea ili akakipige darajani.

Inter imeshakataa ofa mbili za awali za Chelsea kumhitaji straika huyo,na sasa Chelsea inajiandaa kupeleka ofa nyingine ya kiasi kinachokadiriwa Euro milioni 120 wanachoamini kitawashawishi mabingwa hao wa Italia kumuacha mchezaji huyo tegemezi.

Lukaku ameonesha shauku ya kurejea tena darajani baada ya kuondoka mwaka 2014 aliposhindwa kuwika na mabingwa hao wa Ulaya na inaelezwa ameshakubaliana maslahi binafsi na the blues.

Exit mobile version