Site icon Sports Leo

Lusajo Asimamishwa Kmc

Uongozi  wa klabu ya KMC umemsimamisha kwenye timu straika Reliants Lusajo kwa sababu ya utovu wa nidhamu aliouonyesha nyakati tofauti tofauti tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Namungo Fc.

Inadaiwa Lusajo hana furaha ndani ya klabu ya KMC, huku taarifa zikienea kuwa ana mpango wa kurejea katika klabu yake ya zamani ya Namungo.

Hata hivyo mshambuliaji huyo amekua na kiwango kisichoridhisha tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea namungo ambako alikua na wastani mzuri wa kufunga mabao.

Exit mobile version