Wachezaji wa Al Nassr ya Saudia,Mtanzania Clara Luvanga wa timu ya wanawake amekutana ana kwa ana na mshambuliaji wa klabu hiyo kwa upande wa wanaume Cristiano Ronaldo na kufanikiwa kupiga picha ya pamoja ambayo imesambaa katika mitandao ya kijamii hapa nchini.
Clara mchezaji wa zamani wa Yanga Princess alijiunga na klabu hiyo msimu huu akitokea klabu ya Dux Logrono ya nchini Hispania na baada ya takribani miezi mitatu alijiunga na klabu ya Al Nassr ambayo ilivunja mkataba wake na kumnunu moja kwa moja na amefanikiwa kupatia timu hiyo ubingwa wa ligi kuu ya wanawake nchini humo.
Mpaka sasa haijafahamika kama picha hiyo ilipigwa wakati kukiwa na tukio maalumu ama lakini ni jambo rahisi kwao kuonana kwa kuwa wote wanatumikia klabu moja japo wapo timu mbili tofauti zinazomilikiwa na mmiliki mmoja.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mshambuliaji huyo tangu ajiunge na timu hiyo ya wanawake mwaka jana mwezi oktoba amefunga jumla ya mabao 10 katika michezo tisa ya ligi kuu nchini humo na ameisaidia timu hiyo kutwaa kombe la ligi kuu ya wanawake nchini humo.
