Site icon Sports Leo

Lwandamina,Azam Fc Mambo Fresh

Kocha wa zamani wa klabu ya Yanga sc na Zesco United George Lwandamina tayari yupo nchini akiendelea na mazungumzo ya kujiunga na klabu ya Azam Fc yenye makao yake Chamazi jijini Dar es salaam.

Kocha huyo alitua nchini jana na kupokelewa na Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Abdulkarim Amin “Popat” kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya kujiunga na klabu hiyo.

Taarifa za awali zinadai tayari makubaliano yamefikiwa kwa asilimia kubwa huku vikiwa vimebaki vitu vichache dili hilo kukamilika.

Exit mobile version