Site icon Sports Leo

Makambo anukia Yanga sc

Mshambuliaji wa Kidemokrasia ya Kongo Heritier Makambo anatajwa kukaribia kusajiliwa na mabingwa wa kihistoria wa Tanzania klabu ya soka ya Yanga.

Mchezaji huyo alitua nchini siku ya jana akipokelewa na baadhi ya mashabiki wachache wa klabu hiyo waliokuwepo kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere na kuzua hisia kwa mashabiki wa soka kuwa ametua kujiunga na timu hiyo ya zamani aliyoichezea kwa mafanikio makubwa kabla ya kutimkia Horoya ya Guinea.

Akiongea kwa njia ya simu na moja kati ya vituo vya redio Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wananchi wajiandae muda wa wowote kabla ya siku kuisha kwani watatangaza usajili mpya,huku wadau wengi wakiamini ni wa Makambo.

Exit mobile version