Kiungo wa klabu ya Yanga sc Abdulaaziz Makame amejiunga rasmi na klabu ya Polisi Tanzania akitokea klabu ya Yanga sc kwa mkopo wa miezi sita mpaka mwishoni mwa msimu.
Awali makame alisajili na Yanga sc misimu miwili ilkiyopita na anaelekea mwishoni mwa mkataba wake huku sababu kubwa ya kutolewa kwa mkopo ni kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza baada ya kuwasili kwa Mukoko Tonombe.
Makame tayari amesharipoti katika mazoezi ya klabu ya Polisi Tanzania inayojiandaa na mchezo dhidi ya Azam Fc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.