Site icon Sports Leo

Man Utd Yatinga Fainali

Licha ya kufungwa mabao 3-2 klabu ya Manchester United imetinga hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya(Uefa European League) baada ya kuitoa timu ya As Roma kwa jumla ya mabao 8-5.

Mchezo wa awali jijini Rome Man utd ilishinda mabao 6-2 huku mchezo wa pili uliofanyika katika uwanja wa Old Trafford ulimalizika kwa As Roma kushinda mabao 3-2 yakiwekwa kimiani na Eden Dzeko 57′ Bryan Cristante 60′ na Alex Telles aliyejifunga 83′ huku Edson Cavan akifunga kwa upande wa United dakika za 39 na 68.

Man United itakutana na Villareal ya Hispania inayonolewa na Kocha Unai Emery katika fainali itakayofanyika Mei 26.

Exit mobile version