Habari za kuaminika ni kwamba tajiri Yussuph Manji ameanza kurejea katika shughuli za spka taratibu baada ya kulipia kadi yake ya uanachama ya klabu ya Yanga sc ili awe na sifa za kuhudhuria mkutano mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika siku ya Jumapili juni 27.
Tajiri huyo tayari amelipa kadi ya uanachama ya mwaka mzima na atahudhuria mkutano huo kwa mujibu wa watu wa karibu na tajiri huyo.
Klabu ya Yanga sc imepanga kupitisha mabadiliko ya katiba ili kuruhusu kuwa na wawekezaji zaidi ya mmoja huku mashabiki wa klabu hiyo wakitaka mabilionea watatu Manji,Rostam Aziz na Gsm wawekeze.