Site icon Sports Leo

Messi avunja rekodi ya Pele

Mshambuliaji wa Argentina Lionel hatimaye amevunja rekodi ya ufungaji wa mabao Amerika ya Kusini iliyokuwa ikishikiliwa  na gwiji wa soka duniani kutoka Brazil Pele mwenye mabao 77 kwa muda mrefu.

Messi amefikia na kuvunja rekodi hiyo usiku wa kuamkia leo alipoifungia timu yake ya taifa ya Argentina mabao matatu (hat-trick) katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Bolivia kwenye mechi ya kufuzu kombe la dunia Qatar 2022.

Kabla ya mchezo huo La purga alikuwa na mabao 75 mawili nyuma ya Pele lakini baada ya kupiga hat-trick amevunja rekodi hiyo na kufikisha mabao 78 na kuwa kinara.

Argentina ipo nafasi ya pili katika msimamo wa kufuzu kombe la dunia wakiwa na pointi 18 nyuma ya Brazil wanaoongoza wakiwa na pointi 24.

 

Exit mobile version