Mshaambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi anakaribia kujiunga na matajiri wa Ufaransa klabu ya soka ya PSG baada ya kuichagua timu hiyo dhidi ya nyingine.
Baba mzazi wa Messi ambaye pia ni wakala wake Jorge Messi anatarajiwa kusafiri hadi Paris wikiendi hii kukamilisha dili hilo.
PSG kwa sasa inaweka sawa mambo ya kifedha ili kuwepa rungu la FiFA kupitia Finacial Fair Play na endapo wataruhusiwa katika hilo basi watatuma rasmi ofa yao ya mkataba na mshahara kwa kambi ya Messi umnaotarajiwa kuwa ni wa miaka miwili kukiwa na kipengele cha kuongeza mwingine mmoja zaidi.
Uongozi na wachezaji wa PSG wakiongozwa na Neymar anayesukuma zaidi kuungana na rafiki yake huyo wanajiamini zaidi kuwa Messi atajiunga nao.