Site icon Sports Leo

Metacha afungiwa mechi tatu na bodi ya ligi

Golikipa wa mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Yanga sc Metacha Mnata amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya sh 500,000 ( laki tano) kwa kuonyesha ishara ya matusi kwa mashabiki wa klabu hiyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Yanga sc dhidi ya Ruvu shooting na kuzua hasira kwa mashabiki.

Mchezaji huyo alifanya tukio hilo katika mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Ruvu shooting uliofanyka Juni 17,2021 katka dimba la Benjamin Mkapa na kumalizika kwa Yanga kuondoka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi maafande hao kutoka mabatini Pwani.

Mchezaji huyo sasa atakosa michezo yote ya Yanga ilyosalia ikiwamo ule dhidi ya watani wao wa jadi Simba sc utakaofanyika Julai 3,2021.

 

Exit mobile version