Site icon Sports Leo

Metacha Njia Nyeupe Yanga sc

Muda wowote kuanzia sasa, kipa Metacha Mnata anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kukipiga Yanga.

Kipa huyo hivi karibuni aliingia kwenye mgogoro na timu hiyo mara baada ya kuandika ujumbe wa kuaga saa chache baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania uliomalizika kwa Yanga kutoka sare ya bao 1-1.

Inasemekana kipa huyo ndani ya wiki hii kuanzia leo Jumanne, huenda akapewa mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kukipiga Yanga, huku pia akirudishwa kikosi cha kwanza baada ya Farouk Shikalo kuonekana kuwa na makosa ya wazi.

Cc:Sportsextra

Exit mobile version