Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Dodoma jiji Fc Dickson Ambundo amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na klabu ya Yanga sc mara baada ya mkataba wake na klabu hiyo kufika mwisho mwezi juni mwaka huu.
Ambundo alikua anawindwa na klabu kubwa zote nchini lakini Yanga sc wamefanikiwa kumsajili kupitia kwa meneja wa mchezaji huyo aliyelainisha dili hilo huku kiasi hicho cha fedha kikimaliza mjadala ambapo kiungo huyo alikubali kusaini huku akisubiri kutambulishwa tu.
Yanga sc imepata urahisi wa kukamilisha dili hilo huku uwepo wa viongozi wakuu wa klabu hiyo jijini Dodoma katika semina ya mabadiliko kwa wabunge ukirahisisha dili hilo kukamilika pamoja na uhusiano mzuri baina ya mbunge wa Dodoma Anthony Mavunde.