Mahakama Kuu ya Tanzania masjala ya Dar es Salaam inatarajia kusikiliza usuluhishi katika kesi ya kiungo nyota wa Yanga Sc Jonas Mkude ambaye anaidai kampuni ya Mohamed Enterprises (Tanzania) Limited fidia ya Sh 1 bilioni kwa kutumia picha yake katika matangazo ya biashara ya bidhaa zake bila ruhusa yake.
Kesi hiyo ya madai namba 192 ya mwaka 2023ambayo ipo mbele ya Jaji Butamo Philip wa mahakama ambapo ilifika siku ya jana (Jumatatu), Novemba 20, 2023 kwa ajili ya kutajwa ambapo imepangwa kusikilizwa usuluhishi Novemba 27, 2023.
Mbali ya kudai fidia hiyo Mkude ameiomba mahakama hiyo iamuru kampuni hiyo kumlipa mrabaha unaotokana na manufaa ambayo kampuni hiyo imeipata.
Katika madai hayo Mkude aliilalamikia kampuni hiyo kutumia picha yake kutangaza biasha-ra ya huduma zake na bidhaa kupitia mitandao ya kijamii ya Instagram,Facebook na Twitter ikijulikana kama X bila ya kupata ridhaa kutoka kwake.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mkude alijiunga na Yanga sc akitokea Simba sc ambapo julai mwaka huu klabu hiyo ilitangaza rasmi kuachana na kiungo huyo aliyedumu klabuni hapo kwa zaidi ya miaka 10.

