Site icon Sports Leo

Mokoena Anukia Al Ahly

PRETORIA, SOUTH AFRICA - SEPTEMBER 25: Teboho Mokoena of SuperSport United during the DStv Premiership match between SuperSport United and Maritzburg United at Lucas Masterpieces Moripe Stadium on September 25, 2021 in Pretoria, South Africa. (Photo by Lefty Shivambu/Gallo Images)

Kiungo wa klabu ya Mamelod  Sundowns ya Afrika ya Kusini Teboho Mokoena anatajwa kuwa mbioni kujiunga na mabingwa wa klabu bingwa barani Afrika klabu ya Al ahly ya nchini Misri baada ya mabingwa hao kuvutiwa na kiwango cha kiungo huyo katika michuano ya mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Ivory Coast.

Staa huyo kama dili litafanikiwa atajiunga na Al ahly mwishoni mwa msimu na sasa klabu hiyo inajiandaa kutuma ofa rasmi kwa Mamelod juu ya kumnasa staa huyo mzawa nchini Afrika ya kusini ambaye amekua katika kiwango bora kwa sasa.

Mamelod Sundowns wapo tayari kumuuza staa huyo endapo itatokea ofa nono kutoka timu ambazo zinamhitaji staa huyo ambaye alipitia katika akademia ya SuperSports United ya nchini humo huku Mamelod ikimsajili msimu wa 2022/2023 na mpaka sasa ameichezea timu hiyo michezo 42 akifunga mabao 2.

Exit mobile version