Home Soka Morrison Akwama Kuingia Sauzi

Morrison Akwama Kuingia Sauzi

by Sports Leo
0 comments

Viongozi wa klabu ya Simba sc katika kuelekea mechi ya hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika ya kusini walikua na jitihada za kuhakikisha mchezaji Benard Morrison anafanikiwa kuondoa kizuizi cha kuingia nchini humo ili aweze kushiriki katika mchezo huo ambao utatanguliwa na mchezo wa awali April 17 jijini Dar es salaam.

Baada ya Simba sc kugundua kuwa mchezaji huyo haruhusiwi na idara ya uhamiaji kuingia nchini humo zilianza jitihada za kulimaliza suala hilo la mchezaji huyo kupigwa marufuku kuingia nchini humo kutokana na Tabia mbalimbali zisizofaa alizozionyesha kipindi akicheza soka nchini humo.

Inasemekana kuwa mchakato huo umegonga mwamba na sasa mchezaji huyo atasalia nchini baada ya mamlaka ya uhamiaji ya nchini humo kusimamia msimamo wake wa kutomruhusu mchezaji huyo kuingia nchini humo kama ilivyokua hapo awali.

banner

Simba sc imejiwekea malengo ya kuhakikisha inatinga nusu fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa barani Afrika kwa ngazi za vilabu baada ya kuishia hatua ya robo fainali mara mbili hapo awali.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited