Uongozi wa klabu ya Simba sc umethibitisha kuwa, utamkosa winga wao Bernard Morrison kwenye mchezo unaofuata wa ligi kuu dhidi ya Azam fc utakaopigwa katika uwanja wa chamazi kesho.
Kwa mujibu wa uongozi wa Simba sc, Bernard Morrison yuko nchini Ghana kutokana na matatizo ya kifamilia hivyo ataikosa mechi hiyo huku kukiwa hakuna uthibitisho kama ataendelea kukosa na mechi ya watani wa jadi dhidi ya Yanga sc katika fainali ya kombe la shirikisho itakayofanyika julai 25 katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.