Kiungo wa klabu ya Yanga sc Serge Mukoko Tomombe ameitwa katika kikosi cha wachezaji 32 kuelekea katika mechi ya kirafiki dhidi ya Tunisia itakayofanyika juni 10 nchini Tunisia.
Hii ni mara ya pili kwa kiungo huyo kuitwa ambapo mara ya kwanza alifanikiwa kuitumika timu hiyo jumla ya dakika 135 katika michezo ya kirafiki na kimashindano.
Mukoko atakua na kazi ya kugombania namba mbele ya mastaa mbalimbali wanaocheza eneo la kiungo akiwemo Gael Kakuta na wengineo kama Mika Michee, Fabrice Ngoma, Mercey Ngimbi, Paul-Jose Mpoku, Yannick Bangala na Mpanzu Pelly.