Kwa mujibu wa taarifa kutoka Guinea ni kwamba klabu ya Horoya inataka kumnunua kiungo mkabaji wa klabu ya Yanga sc, Mukoko Tonombe na wamejiandaa kuwasilisha Ofa kubwa mezani kwa klabu hiyo ambao ni mabingwa wa ligi kuu mara 27.
Ripoti zinaeleza kuwa Horoya wamejipanga kumsajili Mukoko kwa dau la uhamisho wa dola 200,000 (TSh. 464 milioni) na mshahara mnono wa dola 9000 (Tsh. 18 milioni) kwa mwezi ambao ni takribani mara tatu ya stahiki anazopewa na klabu yake kwa sasa.
Ikumbukwe kiungo huyo amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Yanga sc ambapo ilimsainisha mkataba wa miaka miwili ikimnunua kutoka klabu ya As Vita msimu ulioisha.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.