Site icon Sports Leo

Mukoko Kumfuata Makambo Horoya Fc

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Guinea ni kwamba klabu ya Horoya inataka kumnunua kiungo mkabaji wa klabu ya Yanga sc, Mukoko Tonombe na wamejiandaa kuwasilisha Ofa kubwa mezani kwa klabu hiyo ambao ni mabingwa wa ligi kuu mara 27.

Ripoti zinaeleza kuwa Horoya wamejipanga kumsajili Mukoko kwa dau la uhamisho wa dola 200,000 (TSh. 464 milioni) na mshahara mnono wa dola 9000 (Tsh. 18 milioni) kwa mwezi  ambao ni takribani mara tatu ya stahiki anazopewa na klabu yake kwa sasa.

Ikumbukwe kiungo huyo amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Yanga sc ambapo ilimsainisha mkataba wa miaka miwili ikimnunua kutoka klabu ya As Vita msimu ulioisha.

Exit mobile version