Site icon Sports Leo

Mukoko,Kisinda Wageuka Lulu

Wakala wa wachezaji Tonombe Mukoko na Tuisila Kisinda, Nestroy Mukwale, amethibitisha kwamba amepokea jumla ya ofa tano zinazowahitaji nyota hao wanaoitumikia klabu ya Yanga.
Akiongea na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini Mukwale amesema kati ya ofa hizo tatu zinahitaji huduma ya Mukoko na mbili Tuisila. Amesema ni suala la Yanga tu kuamua kufanya biashara au kubaki nao.

 

Wachezaji hao wamekua na mchango mkubwa kwa Yanga sc msimu huu kiasi cha kuwavutia mawakala mbalimbali duniani huku ikionekana dhahiri klabu hiyo inahitaji kuendelea nao.

Exit mobile version