Site icon Sports Leo

Mwinuke ainukia Simba SC

Winga wa klabu ya soka ya Gwambina Jimmyson Mwinuke amesajiliwa na mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mwinuke mwenye miaka 18 alikipiga Gwambina msimu uliopita na kuonyesha kiwango kizuri kilichowavutia wekundu wa Msimbazi ambao wanaamini atakuja kuwa mchezaji muhimu na mkubwa kwao.

Huu ni muendelezo  wa Simba SC kusajili vijana wadogo ambao wana umri mdogo ikiwa ni mpango wa kuja kuwauza hapo baadae mara baada ya kufanya biashara nzuri dirisha hili kwa kuwauza Chama na Miquissone.

Exit mobile version